Form Five (5) Second Selection / Kidato Cha Tano 2017

  0

  Form Five (5) Second Selection / Kidato Cha Tano

  TAARIFA KWA UMMA Ofisi ya-TAMISEMI inapenda kuwajulisha wananchi juu ya orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwa awamu ya pili kwa mwaka 2017. Wanafunzi hawa wataanza muhula wa kwanza wa masomo tarehe 24 Agosti,2017, na hakutakuwa na mabadiliko yeyote ya shule.

  Wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangiwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti hadi tarehe 08 Septemba 2017 ambayo ndiyo siku ya mwisho ya kuripoti ,atakuwa amepoteza nafasi yake ya masomo. Mwanafunzi mara uonapo jina lako kwenye tovuti ya ofisi ya Rais TAMISEMI kwamba umechaguliwa kujiunga na kidato cha tano inabidi kudowlod fomu ya kujiunga na shule husika kwenye mtandao.

  Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi awamu ya pili mwaka 2017 pamoja na fomu za kujiunga na shule (joining instructions) inapatikana kwenye tovuti ya Ofisi Ya Rais TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz Imetolewa na, Katibu Mkuu Ofisi Ya Rais-TAMISEMI 23 Agosti 2017. Bonyeza hapa kutizama majina ya waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano awamu ya pili 2017.

  BONYEZA HAPA KUANGALIA MAJINA

  For Trending Fashion Styles, Click Here

  LEAVE A REPLY

  Please enter your comment!
  Please enter your name here