Home GOSPEL MUSIC Mbarikiwa – Bwana Uliyewaita – Lyrics – Mp3 Download

Mbarikiwa – Bwana Uliyewaita – Lyrics – Mp3 Download

0
Tenzi Za Rohoni e1527539062366
Tenzi Za Rohoni e1527539062366

Mbarikiwa Mwakipesile – Bwana Uliyewaita – Lyrics

download button

DOWNLOAD AUDIO

1. Bwana uliyewaita watakatifu wako,
wawe mitume wachunga wachunge kundi lako.
Wanyonge na wenye hofu, wakawa mashujaa
Na wapole wa kunena, wasiwe kunyamaa.

2. Hata leo wawataka watakatifu wako,
Nawe wauliza tena ni nani aliyeko,
Atakaye nimtume afundishe vijana,
Nitayari Bwana wangu nitume mimi Bwana.

3. Nitume na mimi Bwana kama ulivyotumwa,
Habari za msamaha na dhambi kutubiwa,
Niwahubiri wakosa na waliopotea
Wokovu u kwake Bwana aliyewafilia.

3. Astahiliye hapana kutamka habari,
Lakini wewe waweza kutufanya tayari,
Neno lako tulijue tupe na Roho wako,
Hayatakuwa ya bure haya maneno yako.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here